Matchday; Yanga vs AS FAR, CAFCL R1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Nov 2025
Matchday; Yanga vs AS FAR, CAFCL R1

Leo Yanga inaanza rasmi safari ya kuisaka robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika itakaposhuka kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuikabili AS FAR ya Morocco.

Ni mchezo wa kwanza kundi B, Wananchi wakikabiliwa na mtihani wao wa kwanza katika kundi linaloaminika kuwa gumu zaidi kuliko mengine.

Ni timu mbili zanye historia ya aina yake katika mashindano ya CAF misimu ya karibuni. Katika misimu mitatu iliyopita Yanga imecheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC) na kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa (CAFCL) huku AS FAR wakicheza robo fainali (CAFCL) msimu uliopita wakiondoshwa kwenye hatua hiyo na mabingwa Pyramids.

AS FAR wamewahi kutwaa taji la CAFCL huku Yanga ikiwa katika mipango ya kulisaka taji hilo kwa mara ya kwanza.

Ni mchezo mgumu lakini Wananchi hawahitaji matokeo tofauti na ushindi ili kuanza vyema mkakati wa kuvuna alama 9 nyumbani.

Yanga imekuwa na muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo ikiwa kambi visiwani Zanzibar kwa siku nne kukamilisha maandalizi.

Itakuwa mara ya kwanza pia kwa wakazi wa visiwani Zanzibar kushuhudia mechi ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, Yanga ikiwasogezea karibu mashindano hayo.

Kila la kheri Yanga, kila la kheri Wananchi...

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’