Kiungo Moussa Balla Conte dakika chache alizopewa katika mchezo dhidi AS FAR alizitendea haki na pengine huo ni mwanzo kwake kupata nafasi zaidi katika kikosi cha kwanza.
Conte amekuwa na mwanzo wa kusuasua Yanga, akikabiliana na presha kubwa kutoka nje ya uwanja.
Usajili wake ulitikisa, awali akihusishwa na Simba kabla ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kuingilia kati na kumnyakua 'juu kwa juu' kutoka klabu ya CS Sfaxien.
Mashabiki walikuwa na matarajio makubwa kwake lakini ni wazi mwanzo wake haukuwa mzuri.
Lakini tangu ujio wa kocha Pedro Goncalves, Conte anaonekana kuimarika zaidi na pengine mashabiki wa Yanga watarajie kuendelea kumuona mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.




ADVERTISE HERE