Yanga yachukua hoteli nzima Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2025
Yanga yachukua hoteli nzima Algeria

Yanga baada ya kutua jijini Algiers jana mchana Novemba 25, 2025, ilisafiri umbali wa takribani kilometa 100 kwa barabara kwenda mji wa Tizi Ouzou ambako ndiko itacheza mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wake, JS Kabylie.

Yanga imefikia hoteli ya Le Relais Vert ambayo timu hiyo itakaa hapo hadi Jumamosi mchana Novemba 29, 2025 itakapoondoka kurejea Tanzania baada ya kumaliza mechi itakayochezwa Ijumaa Novemba 28, 2025.

Inaelezwa Yanga imechukua hotel nzima, haitatumiwa na wageni wengine na itabaki kuwa chini ya Yanga mpaka Jumamosi Novemba 29, 2025 watakapoondoka nchini humo.

Inaelezwa uamuzi wa kuchukua hoteli nzima umelenga kuepuka matukio ya hujuma zikikumbukwa vurugu ambazo Yanga ilifanyiwa kwenye mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa kuamkia Juni 9, 2023 ambapo baadhi ya mashabiki wa USM Alger waliingia mpaka ndani ya hoteli waliyofikia.

Kwenye vurugu hizo, afisa mmoja wa Yanga, Hafidh Saleh alilazimika kukimbizwa hospitali kufuatia kuzidiwa na mafataki yaliyopigwa hotelini hapo.

Yanga itashuka uwanjani Ijumaa wiki hii kwenye mechi ya pili ya Kundi B, itakayopigwa Hocine Aït Ahmed uliopo Tizi Ouzou katika mji wa Boukhalifa, Mkoa wa Kabylia nchini Algeria, wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 50,766 waliokaa.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’