Nyota wa zamani wa Yanga Stephane Aziz Ki na Yacouba Songhne jana walikuwepo dimba la KMC Complex kushuhudia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Licha ya kuondoka Yanga, nyota hao bado wameendelea kuwa na mahusiano mazuri ya Wananchi ikiwa ni ishara ya kuthamini mema waliyofanyiwa na Yanga.
Aziz Ki ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Wydad Athletic, juzi alitinga Avic Town na akapata nafasi ya kushiriki mazoezi.
Hivi karibuni Aziz Ki alipata changamoto ya kiafya visiwani Zanzibar wakati Wydad walipochuana na Azam Fc na kulazimika kulazwa kwa siku chache.
Kwa sasa Ki yuko mapumziko nchini na ametumia wasaa huo kujumuika wa marafiki na waajiri wake hao wa zamani.
Ikumbukwe Aziz Ki ni mume wa Mwanamitindo, Mtanzania Hamisa Mobeto wakifunga ndoa mapema mwaka huu, hivyo hapa ni kama nyumbani pia.