Assink anaitaka namba Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2025
Assink anaitaka namba Yanga

Beki wa kati wa Yanga Frank Assink anaweza kubadili upepo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate uliopigwa uwanja wa KMC Complex jana Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves alimuanzisha Assink nafasi ya nahodha Bakari Nondo Mwanyeto ambaye alikosekana.

Assink aliyesajiliwa na Yanga kwa mkopo kwenye dirisha lililopita akitokea klabu ya Singida BS, alishirikiana vyema na Dickson Job katika safu ya ulinzi akionesha umahiri wake kwenye ulinzi na kuanzisha mashambulizi.

Kulikuwa na tetesi kuwa Yanga ilikusudia kumrudisha Singida BS katika dirisha dogo la usajili baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Lakini ni kama kocha Goncalves ameonyesha mtazamo tofaauti kuhusu beki huyo raia wa Ghana.

Baada ya kucheza kwa dakika 90 dhidi ya Fountain Gate, Assink huenda akapata dakika 90 nyingine katika mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union.

Pengine baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union, Goncalves atakuwa na uamuzi juu ya hatma yake.

Yanga inatarajiwa kumrejesha kikosini Yao Kouassi dirisha dogo litakapofunguliwa n hivyo itahitajika nafasi moja ya nyota wa kigeni.

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’