Yanga kuifuata Coastal Union leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2025
Yanga kuifuata Coastal Union leo

Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam leo Jumamosi Disemba 06 kwa usafiri wa treni kuelekea mkoani Dodoma ambako wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Jamhuri.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya kuwasili mkoani Dodoma watakuwa na muda wa kupumzika na kisha kuhitimisha maandalizi yao katika dimba la Jamhuri.

Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuiunga mkono timu yao katika mchezo wa mwisho kwa mwaka huu 2025.

"Huu ni mchezo wetu wa mwisho kwa mwaka huu 2025 hivyo nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutuunga mkono"

"Ligi itasimama kwa mwezi mmoja na hatutapenda ligi isimame tukiwa tumepoteza mchezo wowote hivyo malengo tuliyojiwekea ni kushinda mchezo huo"

"Wachezaji wetu wako tayari, tulikuwa na changamoto ya 'fartique' katika mchezo uliopita lakini siku hizi mbili naamini zimetosha kufanya 'recovery' na tutarajie kuiona Yanga bora zaidi siku ya Jumapili," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’