Matchday; Coastal Union vs Yanga, NBC PL, Dec 07

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2025
Matchday; Coastal Union vs Yanga, NBC PL, Dec 07

Wananchi Yanga wako mkoani Dodoma ambapo leo majira ya saa moja usiku watashuka uwanja wa Jamhuri kuikabili Coastal Union katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC.

Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kuwania alama tatu mbele ya Wagosi wa Kaya ambao ndio wenyeji wa mchezo huo.

Coastal Union wamehamisha makazi yao kwa muda kutoka jijini Tanga hadi mkoani Dodoma baada uwanja wao wa Mkwakwani kufungiwa.

Mechi inayozikutanisha Coastal Union na Yanga haijawahi kuwa nyepesi. Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves amekiri kuwa kwa historia na rekodi ya mechi za karibuni, vijana wake leo wanapaswa kuwa katika ubora ili kuibuka na ushindi.

Kocha huyo raia wa Ureno tayari ameiongoza Yanga katika mechi tatu za ligi na kuondoka na alama 9, hivyo leo atakuwa akisaka ushindi wa nne na kuihakikishia Yanga kusalia katika nafasi za juu kwenye msimamo wakati ligi ikisimama kwa mwezi mzima kupisha michuano ya Afcon 2025.

Yanga ilitua Dodoma mapema jana na jioni kikosi kikapata nafasi ya kukamilisha maandalizi katika dimba la Jamhuri, Wananchi wakiwa na ari na morali kubwa kuelekea mchezo huo.

Huu utakuwa mchezo wa mwisho kwa Yanga mwaka huu 2025 kwani baada ya mchezo huu ligi itakwenda kusimama kupisha michuano ya Afcon 2025 inayofanyika Morocco.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’