Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amewapa wachezaji wake mapumziko ya wiki moja wakati ligi ikisimama kupisha michuano ya Afcon 2025 itakayoanza mwishoni mwa mwezi huu huko Morocco.
Mapumziko hayo yanawahusu wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa.
Wiki ijayo kikosi cha Yanga kitarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zitakazofuata ambapo baada ya Afcon 2025 kumalizika, Yanga itasafiri Misri kuikabili Al Ahly katika mchezo wa tatu CAFCL kundi B. Timu hizo zitarudiana wiki moja baadae visiwani Zanzibar.
Hizi ni mechi mbili muhimu ambazo zinaweza kuamua hatma ya Yanga kufuzu mapema robo fainali ya CAFCL.
Nyota wa Yanga ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa ni Mohammed Hussein, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Ibrahim Bacca ambao wako timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Djigui Diarra (Mali) na Prince Dube (Zimbabwe)
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kitarejea mazoezini Disemba 15 ambapo watajifua hadi Disemba 20. Kutakuwa tena na mapumziko ya wiki moja kwa ajili ya sikukuu ya Christmass na imu kurejea tena mazoezini Disemba 28