Yanga inatajwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa TRA United, Emmanuel Mwanengo, imefahamika.
Tetesi za Mwanengo (22) kuhusishwa na Yanga zilianza kusikika tangu wiki iliyopita, taarifa za ndani zikidokeza kuwa Yanga tayari imefanya mazungumzo na wasimamizi wa mchezaji huyo na mwafaka umefikiwa.
Hatua iliyobaki ni kumalizana na TRA United ili Mwanengo atue rasmi kwa wananchi kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.
Kabla ya kusajiliwa na Tabora United (sasa TRA United), Mwanengo amewahi kucheza soka la kulipwa Tajistan ambako aliachana kumbukumbu ya kufunga goli bora la mashindano ya Asian cup 2024
Ni mwendelezo wa Yanga kusajili vijana wenye vipaji ili kuwaandaa kuwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Wananchi.
ADVERTISE HERE