Mwaka huu michuano ya kombe la Mapinduzi inarejea kwa kukutanisha klabu baada ya mwaka uliopita kukutanisha timu za Taifa.
Tayari kalenda ya michuano hiyo imetangazwa ambapo inatarajiwa kuanza Disemba 29 hadi Januari 13 ambapo mchezo wa fainali utapigwa.
Taarifa zaidi kuhusu timu zilizoalikwa inatarajiwa kutangazwa siku ya Jumamosi, Yanga ikiwa miongoni mwa timu hizo.
Michuano hii itakuwa sehemu ya maandalizi muhimu wakati huu ambao ligi imesimama kupisha michuano ya Afcon 2025 iyakayoanza kutimua vumbi baadae mwezi huu huko Morocco.
Mara ya mwisho Yanga kutwaa taji la michuano hiyo ni 2021 pale walipowafunga watani zao Simba kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa fainali.
ADVERTISE HERE