Goncalves amewasilisha ripoti ya maboresho - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2025
Goncalves amewasilisha ripoti ya maboresho - Kamwe

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves tayari amewasilisha ripoti yake ya maboresho ya kikosi kuelekea dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa hivi karibuni.

Meneja wa Haari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema tayari uongozi umeanza kuifanyia kazi ripoti hiyo.

"Tayari mwalimu amewasilisha ripoti yake ya maboresho, viongozi wanapambana ili kuhakikisha mapendekezo yake yanafikiwa"

"Mara nyingi kwenye usajili wa dirisha dogo huwa sio rahisi kupata wachezaji bora na daraja la juu lakini uongozi umedhamiria kufanikisha kile alichopendekeza mwalimu, " alisema Kamwe.

Inaelezwa miongoni mwa maeneo ambayo Goncalves amehitaji maboresho ni safu ya ushambuliaji ambapo tayari Yanga inahusishwa na mshambuliaji hatari wa Angola Laurindo Dilson 'DEPU' ambaye ni pendekezo la Goncalves.

Yanga pia inatajwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa TRA United, Emmanuel Mwanengo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’