Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi 2026, Machano Makame Haji jana alitangaza klabu nane zitashiriki Kombe la Mapinduzi 2026, baada ya msimu uliopita mashindano hayo kushirikisha timu za taifa.
Mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Desemba 28, 2025 na kumaliza Januari 13, 2026 ytafnyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Unguja.
Mwaka huu zawadi zimeongezwa ambapo bingwa atakabidhiwa Sh150 milioni, ikiwa ni ongezeko la Sh50 milioni na mshindi wa pili kuramba 100M badala ya 70M
Kwa upande wa Zanzibar timu tatu zitakazoshiriki ni Mlandege ambayo ni bingwa wa mwaka 2023 na 2024, Fufuni na KVZ.
Kutoka Tanzania Bara ni Yanga, Azam, Simba na Singida Black Stars pia kutakuwa na timu alikwa URA ya Uganda.
ADVERTISE HERE