Wananchi wameianza kazi mapema sana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Dec 2025
Wananchi wameianza kazi mapema sana

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazoanza Desemba 21, mwaka huu huko Morocco, mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga, mapema tu wameonyesha dhamira ya kutaka kutetea taji lao kwa msimu wa tano mfululizo.

Yanga imerejea mazoezini baada ya mapumziko ya wiki moja, Wananchi wakianza mawindo ya michuano ya kombe la Mapinduzi itakayoanza visiwani Zanzibar mwishoni mwa mwezi huu.

Mapema tu takwimu za Yanga kwenye ligi zimeonyuesha dhamira ya mabingwa hao wa nchi kuendeleza ubabe wao katika soka la ndani.

Ikiwa imecheza mechi 6, Yanga inaongoza kwa kufunga mabao mengi mpaka sasa, kushinda michezo mingi mfululizo, ndio timu pekee imepata penalti nyingi, imeshinda mechi nyingi nyumbani na kuruhusu mabao machache.

Yanga imefunga mabao 12, yakiwa ni mabao mengi zaidi katika ligi, ikiwa sawa na JKT Tanzania ambayo ina idadi kama hiyo ya mabao.

Hata hivyo, Yanga imecheza mechi sita tu wakati ‘Maafande’ wa JKT Tanzania wameshuka dimbani katika michezo 10 mpaka sasa.

Yanga ina rekodi nyingine safi ya kushinda michezo mingi mfululizo ikiwa imefanya hivyo mara nne. Baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Mbeya City Septemba 30, mwaka huu, Yanga ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, halafu ikatoa kichapo cha mabao 4-1 kwa KMC baadaye ikawafunga Fountain Gate mabao 2-0 na kuidungua Coastal Union ya Tanga goli 1-0.

Yanga pia ina rekodi ya kuwa timu pekee iliyopata penati nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka sasa, zote ikizitumia.

Imepata penalti mbili, kati ya nane zilizotolewa na waamuzi kwenye Ligi Kuu na zote ikiziweka kwenye kamba. Ilipata penalti yake ya kwanza Novemba 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam ilipocheza dhidi ya wenyeji, KMC mfungaji akiwa ni straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR Congo), Andy Boyeli, vigogo hao wakishinda mabao 4-1.

Yanga ilipata penalti nyingine Desemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa KMC Complex ilipowakaribisha Fountain Gate, ikafungwa na Prince Dube, Yanga ikishinda mabao 2-0.

Kama vile haitoshi, Yanga ndiyo timu pekee iliyoshinda michezo mingi ya nyumbani msimu huu mpaka sasa, ikifanya hivyo mara nne, kwa kuichapa Pamba Jiji mabao 3-0, Mtibwa Sugar mabao 2-0, KMC mabao 4-1 na Fountain Gate, mabao 2-0.

Mabingwa hao watetezi ndiyo timu pekee iliyoruhusu mabao machache, ikiruhusu bao moja tu, ilifanya hivyo Novemba 9, mwaka huu ilipocheza dhidi ya KMC na kushinda mabao 4-1.

Katika msimamo wa ligi, Yanga yenye pointi 16 iko kwenye nafasi ya pili ikilingana pointi na Pamba Jiji huku JKT Tanzania wakiongoza na pointi zao 17 kibindoni.

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’