Yanga yatupwa kundi C kombe la Mapinduzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2025
Yanga yatupwa kundi C kombe la Mapinduzi

Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Disemba 28 kwa mchezo kati ya Singida Black Stars dhidi ya Mlandege.

Yanga ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo itakayokutanisha timu 10 badala ya 8 zilizotangazwa awali.

Timu hizo zimepangwa katika makundi matatu ambapo kundi A linaundwa na timu nne huku makundi B na C yakiundwa na timu tatu tatu.

Mlandege Fc, Singida BS, Azam Fc na URA zinaunda kundi A ambapo katika kundi hilo timu mbili zitakazomaliza kwenye nafasi mbili za juu zitafuzu nusu fainali.

Kundi B linaundwa na timu za Simba, Mwembe Makumbi na Fufuni huku Kundi C likiundwa na Yanga, TRA United na KVZ

Timu zitakazomaliza nafasi ya kwanza kundi B na C zitafuzu hatua ya nusu fainali.

Yanga inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya KVZ Januari 04 na kuhitimisha mechi ya pili ya makundi Januari 06 dhidi ya TRA United.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’