Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi 'Jeshi'.
Yao amekuwa nje kwa takribani miezi sita akiuguza jeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwishoni mwa msimu uliopita.
Tayari nyota huyo kutoka Ivory Coast amepona na kurejea mazoezini sasa akisubiri kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili ifikapo Januari 1 ili aweze kusajiliwa rasmi.
Wananchi wanasubiri kwa hamu urejeo wake ambapo sasa anakwenda kumpa changamoto Israel Mwenda aliyejimilikisha nafasi ya beki wa kulia katika kipindi chote ambacho Yao alikosekana.
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
HAPPY BIRTHDY YAO...!
ADVERTISE HERE