Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kiungo fundi wa Yanga Mohamed Doumbia maarufu 'AI'.
Doumbia ni miongoni mwa sajili mpya zilizokamilishwa na Yanga katika dirisha lililopita, akitua kuchukua nafasi ya Stephane Aziz Ki aliyetimkia Wydad AC.
Bado unaweza kusema Wananchi hawajashuhudia ubora wake uliompa sifa nyingi wakati anajiunga na Yanga.
Doumbia ameendela kuzoea mazingira ya ligi kuu ya Tanzania Bara pengine ni suala la muda tu ataonyesha thamani yake halisi.
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
HAPPY BIRTHDAY DOUMBIA...!
ADVERTISE HERE