Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ni kama ametoa 'code' ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa Vipers Fc Allan Okello kutoka Uganda.
Hersi amesema yeye ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo na mara kadhaa alikwenda Uganda kumfuatilia tangu mwaka 2019.
Bila ya kumtaja, Hersi amesema kwenye dirisha dogo au dirisha la Juni, kuna mchezaji atamsajili kutoka Uganda.
"Nampenda sana Allan Okello, nlimfuatilia kwa muda mrefu kabla hajaenda Algeria. Nakumbuka mwaka 2019 nilienda Uganda kumfuatilia yeye, Bobosi na Mustapha Kizza"
"Niwaambie mashabiki wa Yanga, kama sio Januari basi Juni tutamleta mchezaji kutoka Uganda," alisema Hersi.
Okello anatajwa kuwa mchezaji aliyepewa kipaumbele kusajiliwa na Yanga ili kuongeza nguvu eneo la kiungo cha ushambuliaji (namba 10)