Timu za taifa za Uganda na Tanzania jana ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Kundi C, katika michuano ya AFCON 2025.
Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti huku Uche Ikpeazu akiisawazishia Uganda.
Matokeo hayo yameiweka njia panda Stars katika malengo ya kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
Stars itahitimisha hatua ya makundi kwa kuumana na Tunisia katika mchezo ambao Tanzania itahitaji ushindi ili kutinga hatua ya mtoano.
Tunisia jana ilipoteza dhidi ya Nigeria kwa kuchapwa mabao 3-2, ikisalia na alama tatu katika nafasi ya pili.
Kimahesabu Tunisia, Tanzania na Uganda zote zina nafasi ya kutinga mtoano lakini Tunisia ikiwa na nafasi zaidi ikihitaji alama moja tu.
Nigeria tayari imetinga hatua ya mtoano baada ya ushindi dhidi ya Tunisia.