Klabu ya Yanga imefungua mazungumzo na Singida Black Stars wakimtaka kiungo Mohammed Damaro kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu, imefahamika.
Yanga inasaka kiungo mkabaji mwingine ambaye huenda akachukua nafasi ya Moussa Balla Conte ambaye mwanzo wake na Wananchi umekuwa wa kusuasua.
Damaro alikuwa kwenye rada za Yanga tangu dirisha lililopita lakini Wananchi walishindwa kukamilisha usajili wake kwa wakati.
Ni wakati mzuri kwa pande zote mbili kwani hata Damaro mwenyewe amehitaji changamoto mpya baada ya kutokuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.
Singida BS ilimsajili Khalid Aucho ambaye ni chaguo la kwanza eneo la kiungo mkabaji.
ADVERTISE HERE