Winga kiraka wa Yanga Denis Nkane anakamilisha mchakato wa kujiunga na TRA United kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu, imefahamika.
Benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha mkuu Pedro Goncalves limependekeza baadhi ya wachezaji kutolewa kwa mkopo ili wapate nafasi ya kucheza katika klabu nyingine.
Nkane ni miongoni mwa wachezaji hao ambapo kuna uwezekano mkubwa akajiunga na TRA United visiwani Zanzibar.
Yanga itaelekea Zanzibar leo kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo itashuka dimbani Jumapili, Januari 04 kuikabili KVZ.
ADVERTISE HERE