Kouma aongeza idadi ya majeruhi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
5 Jan 2026
Kouma aongeza idadi ya majeruhi Yanga

Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Lassine Kouma hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili TRA United katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi kombe la Mapinduzi.

Kouma aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya KVZ ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema Jamatatu, Goncalves pia aliwaataja Celement Mzize, Mudathir Yahya na mlinda lango Aboubakar Khomein pia watakosekana/

“Tutawakosa wachezaji kadhaa akiwemo Clement Mzize ambaye anaendelea na mazoezi ya kuweka mwili sawa tangu arejee kutoka Majeruhi, pia Mudathir ambaye ana siku chache tu za kurudi uwanjani, Kadhalika Lassine Kouma na Golikipa wetu Khomein ambao na wao wapo kwenye majeruhi,” alisema

Goncalves ameweka wazi mpango mkakati wake kuelekea mchezo huo ambapo ameahidi kuendelea kuwapatia nafasi wachezaji wote ukiwa ni mpango wake wa kuimarisha viwango vya wachezaji wote.

“Tumekamilisha mazoezi ya kujiandaa na mchezo muhimu dhidi ya TRA, Dhamira yetu kubwa ni kuwa tayari kufanya vizuri kila mchezo, haijalishi wenzetu wamepata muda mrefu wa kujiandaa kuliko sisi lakini ni lazima tuwe tayari kwaajili ya kushinda, Ninaamini tutatinga hatua ya nusu fainali baada ya mchezo wa kesho,” alisema.

Yanga inahitaji ushindi au sare ili kutinga nusu fainali.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →