Hersi atua Uganda, Okello ni suala la muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jan 2026
Hersi atua Uganda, Okello ni suala la muda

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said yuko nchini Uganda kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Allain Okello anayeitumikia klabu ya Vipers Fc, imefahamika.

Taarifa kutoka Uganda imedokeza kuwa mapema leo Hersi alikuwa na mazungumzo na Rais wa klabu ya Vipers Fc Laurence Mulindwa kwa ajili ya kuhitimisha mchakato wa usajili wa nyota huyo.

Vipers Fc waligomea ofa ya kwanza ya Yanga, wakihitaji dau nono zaidi ili kumuachia mchezaji huyo bora zaidi ligi kuu ya Uganda kwa sasa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Hersi aliweka wazi dhamira yake ya kumsajili Okello katika dirisha hili na hata kama itashindikana sasa, atamsubiri dirisha kubwa wakati huo mkataba wake na Vipers Fc utakuwa umemalizika.

Habari njema ni kuwa baada ya mazungumzo baina ya viongozi hao, mwafaka umefikiwa na sasa kinachosubiriwa ni kukamilishwa kwa mchakato wa usajili.

Mazungumzo binafsi kati ya Okello na Yanga yalikamilika mapema, kilichokuwa kinasubiriwa ni ruhusa kutoka klabu yake ili aweze kutua Yanga.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’