Mauzo ya Okello yavunjwa rekodi Vipers Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jan 2026
Mauzo ya Okello yavunjwa rekodi Vipers Fc

Baada ya Yanga kukamilisha uhamisho wa aliyekuwa winga wa Vipers na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Allan Okello timu hiyo kwa sasa imevunja rekodi ya usajili ya kikosi hicho na kuivuka iliyokuwa inashikiliwa na Cesar Lobi Manzoki.

Okello amekamilisha usajili huo baada ya mazungumzo ya pande mbili kati ya Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said na Lawrence Mulindwa wa Vipers, ambapo wawili hao walikutana tangu wiki iliyopita jijini Kampala Uganda ili kukamilisha dili hilo.

Baada ya dili hilo kukamilika, Yanga imetoa kiasi cha Sh740 milioni ambazo ni $300,000 sawa na UGX1 bilioni za Uganda, akiwa ni nyota wa pili ghali kuuzwa na Vipers, baada ya kiungo mshambuliaji, Farouk Miya aliyejiunga na Standard Liege.

Miya aliyejiunga na Standard Liege ya Ubelgiji mwaka 2016, ndiye mchezaji ghali zaidi kuuzwa na Vipers, ambapo kiungo huyo mshambuliaji aliuzwa kwa Sh986 milioni, ikiwa ni $400,000 ambazo kwa fedha za Uganda ni sawa na UGX1.4 billion.

Nyota mwingine anayefuatia kwa kuuzwa fedha nyingi ni mshambuliaji, Cesar Manzoki aliyeuzwa China mwaka 2022 na kujiunga na kikosi cha Dalian Professional, ambapo Vipers iliingiza Sh493 milioni, ambazo ni $200,000, sawa na UGX721 milioni.

Kwa maana hiyo, Farouk Miya ndiye mchezaji anayeendelea kushikilia rekodi ya kuuzwa kwa kiasi kikubwa cha fedha akitoka Vipers, akifuatiwa na Okello aliyejiunga na Yanga na kumpiku pia, Manzoki aliyekuwa akihusishwa na Simba mara kwa mara.

Okello aliyetamba na timu mbalimbali zikiwemo za KCCA ya Uganda na Paradou AC ya Algeria, anaungana na nyota wengine pia wapya waliosajiliwa dirisha hili dogo, baada ya kiungo, Mohamed Damaro aliyetokea katika kikosi cha Singida Black Stars.

Wengine ni, Emmanuel Mwanengo aliyekuwa TRA United zamani Tabora United na mshambuliaji, Laurindo Dilson Maria Aurelio 'Depu' raia wa Angola, anayetua ndani ya kikosi hicho akitokea Radomiak Radom ya Poland, ili kwenda kuongeza nguvu mpya.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’