Kikosi cha Yanga jioni ya leo saa 10:30 watashuka uwanja wa Gombani huko Pemba kuikabili Azam Fc katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi.
Ni nafasi muhimu kwa Wananchi kuandikisha taji la kwanza kwa mwaka huu 2026.
Lakini pia ni nafasi kwa kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves kuandikisha taji lake la kwanza tangu alipojiunga na mabingwa hao wa nchi akichukua nafasi ya Romain Folz.
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali, Azam Fc haijawahi kuwa timu nyepesi kila inapokutana na Yanga.
Yanga ilikamilisha maandalizi yake jana Unguja na leo sa 4 asubuhi itawasili Pemba tayari kwa mtanange huo ambao ni sehemu za shamrashamra ya kumbukumbu ya Mapinduzi matakatifu ya Zanzibar.
ADVERTISE HERE