FT : Yanga 6-0 Mashujaa Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
19 Jan 2026
FT : Yanga 6-0 Mashujaa Fc

Yanga leo imetoa onyo kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya NBC ikiifumua Mashujaa Fc mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Wananchi walitawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza lilikuwa ni suala la mabao mangapi Yanga ingefunga katika mchezo huo.

Mohamed Damaro aliyefungua kalamu ya mabao mapema tu kwenye dakika ya 7 akimaliza kwa kichwa mpira ulioparazwa na Dickson Job.

Pacome Zouzoua na Duke Abuya wakaongeza mawili kabla ya mapumziko na kuwapeleka Wananchi mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Yanga iliendeleza ilipoishia kipindi cha kwanza na kuongeza mabao mengine matatu kupitia kwa Prince Dube, Mudathir Yahya na  Laurindo Dilson 'Depu' aliyeingia kipindi cha pili.

Depu alimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango Erick Johora baada ya shuti la Allan Okello kupitia mpira wa adhabu.

Sio kufunga tu, Depu pia alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mudathir Yahya.

Ni ushindi mnono unaoipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi. Ni salamu kwa wapinzani, wajipangeeee..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →