Goncalves apania kuwaduwaza Al Ahly Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2026
Goncalves apania kuwaduwaza Al Ahly Misri

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema wachezaji wake wana morali kubwa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Ijumaa, Januari 23 huko Misri.

Akizungumza na wanahabari jana muda mfupi kabla ya kuondoka nchini, Goncalves alisema licha ya kukabiliwa na safari ndefu lakini wanakwenda Misri wakiwa na ari kubwa.

"Hatutakuwa na muda mrefu wa maandalizi lakini nikwambie wachezaji wangu wana ari kubwa kuelekea mchezo huo"

"Tutasafiri kwa ndege hadi Cairo kisha tutapanda basi hadi mji wa Alexandria, muda ni mfupi lakini tumeshajiandaa hapa"

"Sasa tuna timu iliyoimarika zaidi ambayo inatupa nafasi ya kushindana na timu bora kama Al Ahly. Wachezaji wote tulisafiri nao wako tayari na tunakwenda kuipambania nembo ya Yanga," alisema Goncalves.

Yanga itasafiri kwa takribani masaa tisa ambapo masaa  matano watakuwa angani hadi Cairo ambapo hapo watachukua usafiri wa basi kuelekea mji wa Alexandria takribani masaa manne.

Mchezo dhidi ya Al Ahly utapigwa Ijumaa, saa 1 usiku kwa saa za Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’