Kikosi cha Yanga kimeondoka Alexandria saa 9 Alasiri wakirejea Cairo kisha kuunganisha safari ya kurejea Dar es salaam baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly uliopigwa uwanja wa Borg EL Arab jana na Yanga kupoteza kwa mabao 2-0.
Mapema leo kabla ya kuanza safari, kikosi kilifanya program ya mazoezi asubuhi ambapo safari yao hadi kufika Dar itachukua takribani masaa 8.
Kikosi kinatarajiwa kuwasili Dar es salaam Alfajiri ya kesho Jumapili.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema tayari wametaarifiwa na Bodi ya ligi juu ya mechi ya kiporo ya ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambayo itapigwa uwanja wa KMC Complex siku ya Jumanne, saa 1 usiku.
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea visiwani Zanzibar kukamilisha maandalizi kabla ya kuikabili Al Ahly Januari 31 katika uwanja wa New Amaan Complex.