Klabu ya Marumo Gallants inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini, imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mohamed Doumbia.
Doumbia ametua Marumo kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu.
Kiungo huyo aliondolewa kwenye mipango ya kikosi cha Yanga katika dirisha hili ambapo alipewa nafasi ya kutafuta timu baada ya kugomea mpango wa kutua Singida BS.
Doumbia Anaungana na Celestin Ecua kuwa wachezaji wa kigeni waliotolewa kwa mkopo Ecua akitua JS Kabylie.
ADVERTISE HERE
