Jumamosi, Januari 31 Yanga ina jambo lake pale dimba la New Amaan Complex itakapoikabili Al Ahly katika mchezo wa raundi ya nne kundi B michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Wananchi wataingia katika mchezo huo wakiwa na ajenda moja tu, ushindi ambao utawaweka katika nafasi nzuri ya kukata tiketi ya hatua ya robo fainali.
Yanga imetangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni.

ADVERTISE HERE