Mchezo wa raundi ya tano ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) kundi B umemalizika kwa wenyeji AS FAR kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.
Kwa takribani dakika 85 Yanga waliweza kulilinda lango licha ya mashambulizi mfululizo kutoka kwa AS FAR.
Lakini kosa moja moja liliigharimu Yanga AS FAR wakifunga bao lao baada ya walinzi kuchelewa kuondoa hatari langoni.
Ni Yanga iliyotengeneza nafasi adimu zaidi kwenye kipindi cha pili lakini Prince Dube hakufanikiwa kutumia nafasi mbili huko Clement Mzize aliyeingia kuchukua nafasi y Pacome nae akikosa.
Matokeo hayo yanaipa mtihani Yanga kushinda mchezo wa mwisho nyumbani dhidi ya JS Kabylie huku wakiomba Al Ahly ipate ushindi dhidi ya AS FAR katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi.
Mpaka sasa Al Ahly tayari imefuzu robo fainali ambapo mechi yao ya mwisho itakuwa kwa ajli ya kujihakikishia nafasi ya kwanza.
Yanga itahitaji kushinda angalau mabao mawili katika mchezo dhidi ya JS Kabylie.