Kiungo wa Yanga Mohamed Damaro Camara anatarajiwa kukosa mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie utakaopigwa Jumapili, Februari 15 uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Camara ana kadi tatu za njano ambazo kwa mujibu wa kanuni zinamnyima sifa ya kucheza mechi hiyo.
"Damaro hatakuwa sehemu ya mchezo kwa sababu ya kadi za njano. Ana kadi tatu za njano, moja akitoka nayo Singida BS"
"Hivyo kwa mujibu wa kanuni yeye anapaswa kukosa mchezo huo na ndio maana hajasafiri na wachezaje wengine kuja hapa Zanzibar"
"Lakini wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo huo dhamira yetu iliwa kupata ushindi na tufuzu kwa kishindo kutoka kundi B," alisema Kamwe
Klabu ya JS Kabylie inatarajiwa kuwasili nchini leo tayari kwa mtanange huo ambao dakika 90 zitaamua hatma ya Yanga kuelekea robo fainali.