Yanga imeanza vyema hatua ya 64 bora kombe la CRDB ikiichap Cosmopolitan mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Winga Buba Jammeh ndiye aliyepeleka kilio Cosmo akifunga mabao yote ya Yanga mapema kwenye kipindi cha kwanza.

Ulikuwa mchezo wa vipindi viwili ambao Yanga ilicheza kwa kasi na kutengeneza nafasi nyingi kwenye kipindi cha kwanza lakini Wananchi walipunguza kasi kpindi cha pili na kufanya mchezo huo kupooza.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves alifanya mabadiliko ya kikosi chake akiwapumzisha wachezaji ambao wametumika sana msimu huu huku akiwapa nafasi nyota wengine.
Yanga imetinga hatua ya 32 bora ikiungana na timu nyingine zilizofuzu kwenye hatua hiyo.
ADVERTISE HERE