Goncalves awaonya wachezaji wasiojituma Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Feb 2026
Goncalves awaonya wachezaji wasiojituma Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kutakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na ratiba ngumu iliyo mbele yao, huku akiwaonya wachezaji wa kikosi hicho kuacha kuridhika wapatapo nafasi, akisisitiza kila mmoja anapaswa kuonyesha kitu pindi akiaminiwa.

Goncalves aliyasema hayo baada ya mchezo wa kombe la CRDB dhidi ya Cosmopolitan katika hatua ya 64 Bora ya Kombe la Shirikisho (FA) iliyochezwa Februari 18, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex Yanga ikishinda 2-0.

Pedro amesema wachezaji waliocheza wamepata kipimo kizuri kutoka kwa wapinzani kwani ulikuwa mchezo mzuri kutokana na Cosmopolitan kujiandaa vizuri kuonyesha ushindani, huku akilia na wachezaji wake kukosa mwendelezo mzuri wa ubora.

“Licha ya timu kupata matokeo, lakini haikuwa vizuri kama tulivyokuwa tunatarajia, mchezaji hata asipopata mechi mara kwa mara kile anachokipambania akiwa katika uwanja wa mazoezi anatakiwa kukionyesha kwenye mechi ya ushindani ili kunipa nafasi ya kumuamini zaidi, wengi wamecheza kawaida, hii siyo nzuri.

“Tuna mechi nyingi na ratiba siyo rafiki kwetu, ni muda wa wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza huku wengine wakitumika mara kwa mara kwa mechi ngumu tulizocheza za Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo tunawapumzisha ili kurudisha utimamu kabla ya kumkabili mpinzani wetu Simba,” alisema Pedro.

Alisema kila mchezaji aliyesajiliwa Yanga ana umuhimu wake na atatumika kulingana na mahitaji ya mechi husika, hivyo anaheshimu uwezo wa kila mmoja lakini anawakumbusha kuipa thamani hata dakika moja wanayoipata kuitumikia timu hiyo ambayo ina malengo makubwa msimu huu.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’