Mashabiki wa Yanga bado wanamsubiri kiungo wao mshambuliaji Allan Okello afungue akaunti ya mabao akiwa hajafanikiwa tangu ajiunge na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
Tangu atue Yanga, Okello ameanza kuonyesha makali yake kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Pedro Goncalves ambaye mara kadhaa amemsifu Mganda huyo kuwa ana kipaji kikubwa.
Goncalves anamtumia Okello katika maeneo tofauti kama kiungo mshambuliaji anayetokea pembeni na wakati mwingine akimtumia eneo la namba 10 akibadilishana na Mudathir Yahya.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wasiingizwe kwenye mtego na wachambuzi kumjadili mchezaji huyo kwani hakuna mashaka juu ya uwezo wake uwanjani.
Kamwe amesema hana wasiwasi na Okello, ni suala la muda tu atafungua akaunti yake ya mabao.