Goncalves azitaka alama tatu mechi dhidi ya JKT Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Feb 2026
Goncalves azitaka alama tatu mechi dhidi ya JKT Tanzania

Licha ya ugumu wa ratiba, kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema vijana wake wanapaswa kupambana na kuhakikisha wanachukua alama tatu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania.

Kesho Jumatano, Februari 25 Yanga itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex, saa 10 jioni.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo,Goncalves alisema hawajapata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo lakini anaamini wachezaji wake wako tayari na wataipambania nembo ya Yanga.

“Ukweli ni kwamba tuna muda mchache sana kujiandaa na mchezo ujao. Tunapaswa kujiandaa vyema kuhakikisha tunapata matokeo licha ya changamoto ya muda."

"Tuna msururu wa mechi nyingi ambazo ni ngumu. Mechi ya Namungo tulikumbana na mazingira magumu lakini tulipata matokeo. Lakini sisi ni timu kubwa tunapaswa kukabiliana na kila kikwazo”

“Wapinzani wetu JkT wamepata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo wetu. Ni timu nzuri ambayo wanayo hamasa ya kutosha."

"Tunapaswa kubaki kwenye lengo letu na kupata alama tatu. Utakuwa mchezo mzuri sana. Tuna maeneo machache ya kuboresha kwenye kikosi chetu. Kama tunataka kufanya vizuri lazima tuboreshe changamoto zetu kimbinu na kiufundi,” alisema Goncalves

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mshambuliaji Emmanuel Mwanengo amesema wanatambua ugumu wa mchezo ulio mbele yao na watakwenda kupambana kupata alama tatu licha ya kukabiliwa na ratiba ngumu.

“Tuna ratiba ngumu kidogo. Tumefika jana, hatujapata muda wa kutosha wa kupumzika. Lakini unapokuwa mchezaji una wajibu wa kuwa tayari muda wowote. Tunaenda kufanya mazoezi ya mwisho leo na naamini wachezaji wote morali ipo juu.”

"JKT ina wachezaji wenye uzoefu ambazo wamecheza timu kubwa. Huenda tukawa na mchezo mgumu zaidi ya uliopita. Uchezaji wao unakaribiana na sisi kwa maana ya kumiliki mpira."

"Hii ni Yanga, kila mchezo kwetu ni fainali. Hatupaswi kudondosha alama yoyote katika mazingira yoyote. Naamini tutafanya zaidi ya mchezo uliopita. Tunawaomba sana mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja. Matokeo ya mchezo uliopita tunafahamu haturidhishwa na kiwango, hivyo tunaahidi matokeo mazuri na ushindi,” alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’