Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi za viporo ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa uwanja wa KMC Complex kuikabili JKT Tanzania.
Unaweza kusema ni vita ya juu ya msimamo kwani zinakutana timu ambazo ziko kwenye nafasi mbili za juu.
JKT Tanzania ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 28 baada ya mechi 16 huku Yanga wakifuatia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 25 baada ya mechi 9.
Yanga ina nafasi ya kupanda kileleni mwa msimamo kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Licha ya kusema vijana wake wanakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo, kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na dhamira moja tu, kuondoka na alama zote tatu.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni Yanga ikiweka hadharani viingilio;
