Mabingwa wa Zanzibar, JKU wameyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kulazwa mabao 3-0 na Gor Mahia katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Afraha, Nakuru Kenya.
Mabao ya George Odhiambo, Walusimbi na Meddy Kagere yaliihakikishia Gor Mahia, mabingwa watetezi wa michuano hiyo kutinga hatua ya nusu fainali na kuiacha JKU ikiungana na Yanga kurudi nyumbani mapema.
Ni Simba na Singida United pekee zilizobaki kwenye michuano hiyo inayoshirikisha timu nne kutoka Tanzania na nne kutoka Kenya.
Simba inacheza kesho Jumatatu dhidi ya K. Sharks wakati Singida United itashuka dimbani Jumanne kucheza na AFC Leopards.
Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 30,000 sambamba na kupata tiketi ya kwenda kucheza na Everton nchini Uingereza.

ADVERTISE HERE