Tunawaheshimu Simba, wana timu nzuri - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2026
Tunawaheshimu Simba, wana timu nzuri - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanatambua mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili March 1 katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar utakuwa mgumu.

Kamwe amesema kwa sasa Simba wana kikosi bora hivyo wanapaswa kujiandaa vyema huku wakitambua wanakabiliwa na mpinzani mgumu mbele yao.

"Nisema ukweli, wapinzani wetu Simba wana timu nzuri na wamesajili vizuri sana. Hawa watu wametoka kuangusha pointi kwenye mchezo uliopita lakini ukiangalia mechi yao walicheza vizuri, walikosa bahati tu"

"Mimi huwa naangalia mechi za Simba, nataka nijifunze vitu vingi kutoka kwao. Wamefanya usajli mzuri dirisha dogo," alisema Kamwe.

Kamwe amesema Yanga inaendelea na maandalizi yake huku akimtaja kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua kuwa anaendelea kuimarika, hatma yake itafahamika baada ya mazoezi ya hizi siku mbili zilizobaki.

Kuhusu Prince Dube, Kamwe amesema alicheza mechi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania akiwa majeruhi hivyo nae anaendelea kuimarika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’