Dabi ya kwanza kwa Goncalves

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2026
Dabi ya kwanza kwa Goncalves

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves leo anakwenda kucheza dabi yake ya kwanza ya Kariakoo tangu arithi mikoba iliyoachwa na Romain Folz ambaye aliongoza mechi za mwanzoni mwa msimu ukiwemo mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Mtangulizi wake Folz aliwafunga Simba na kubeba Ngao ya Jamii, akihakikisha Yanga inashinda mechi ya sita mfululizo dhidi ya Simba.

Leo Goncalves atakuwa na nafasi ya kuendeleza ubabe dhidi ya wapinzani wao wa jadi kwa kuibuka na ushindi na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi.

Kocha huyo raia wa Ureno anafahamu kile ambacho timu yake inapaswa kufanya leo ili kuibuka na ushindi.

Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu kuona kikosi atakachoanza nacho siku ya leo ingawa kwa kufuatilia mechi zilizopita, unaweza kutabiri ataingiaje katika mchezo huo.

Ni wazi safu yake ya ulinzi haitakuwa na mabadiliko makubwa Djigui Diarra akitarajiwa kuendelea kulinda milingoti mitatu ya lango akisaidiwa na Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Dickson Job na Ibrahim Bacca.

Mohamed Damaro huenda akatumika katika eneo la kiungo wa ulinzi huku Duke Abuya akisogea namba 8 na pengine Allan Okello kuanza eneo la kiungo cha ushambuliaji (namba 10) na Maxi Nzengeli akitokea pembeni upande wa kulia.

Bado hakuna uhakika kama Pacome Zouzoua ataanza mchezo huo kwa kuzingatia utimamu wake wa mwili lakini kama hatakuwa tayari, Prince Dube na Depu wanaweza wakapewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji kama walivyofanya kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Silaha kubwa ya Yanga katika mchezo wa leo ni kasi kwa kuzingatia safu ya ulinzi ya Simba wachezaji wake hawana kasi.

Kama vijana wa Goncalves watakuwa na ufanisi mbele ya lango kama walivyofanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania, huenda Wananchi wakaandika rekodi nyingine kwa kuibuka na ushindi visiwani Zanzibar.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
47m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’