Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Singida BS mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Airtel, Mtipa Singida.
Alikuwa ni Prince Dube aliyeibuka shujaa katika mchezo huo akifunga bao moja na kuhusika kwenye mabao mengine mawili.
Dube alifunga bao la uongozi dakika ya 41 akimalizia krosi ya Maxi Nzengeli. Dakika ya 45 Dube alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na Chukwu mwamuzi akiamuru mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Allan Okello.
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kuongeza bao la tatu kupitia kwa Mudathir Yahya akimalizia mpira uliotemwa na Metacha Mnata baada ya shuti la Dube.
Yanga ilicheza mchezo huo kwa tahadhari na 'tempo ya chini' wakikabiliana na ratiba ya mechi mfululizo.
Wananchi wamefikisha alama 32 baada ya mechi 12, wakizidi kusimika juu ya msimamo wa ligi




