Bodi ya Ligi (TPLB) imeurudisha mchezo wa ligi kuu kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Kulikuwa na mkanganyiko wa ratiba baada ya Tanzania Prisons hapo jana kutangaza kuwa watacheza mchezo huo uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Bodi ya ligi ndio yenye mamlaka ya mwisho kuamua wapi mchezo huo utapigwa baada ya kufungia uwanja wa Sokoine.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho kuelekea Dodoma tayari kwa mtanange huo.
ADVERTISE HERE