Tinocco ahusishwa kurejea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2018
Tinocco ahusishwa kurejea Yanga
Mlinda mlango wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinocco ameaga ndani ya kikosi hicho na msimu ujao wa ligi kuu anadaiwa atakuwa kwenye timu moja mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Tinocco ambaye amesajiliwa na Mtibwa akitokea Yanga na kupata msasa chini ya Kocha Patrick Mwangata anayetwaja kuwa bora katika kuwanoa walinda mlango.

Inadaiwa yupo kwenye mazungumzo na timu tofauti ikiwemo Simba lakini Yanga ndiyo wako kwenye nafasi ya kumchukua mchezaji huyo na muda wowote atasaini.

Jamaa wa karibu wa Yanga amesema, kikosi hicho kinamuhitaji mchezaji huyo kwa nguvu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

"Zipo timu nyingi zinazomuhitaji lakini Yanga ni miongoni mwa timu hizo na inamuhitaji kwa nguvu zote, ingawa zipo pia KMC na nyingine,"alifafanua jamaa huyo.

Hata hivyo, alipoulizwa Tinocco amesema: "Mimi nimeaga Mtibwa lakini si kwa sababu naenda Yanga, kuna mipango yangu mingine ninayotegemea kuifanya kama hizo habari zipo tusubiri tuone."

Tinocco amesema, kuna timu tofauti zinazohitaji huduma yake hasa baada ya kusikia amemaliza mkataba wake na Mtibwa lakini hawezi kuweka wazi hadi mipango itakapokamilika.

Baada ya Benno Kakolanya kumaliza mkataba wake, hakuna uhakika kama ataongezewa mkataba mwingine huku kipa Youthe Rostand naye akiwa na hatihati ya kuendelea kubaki Jangwani.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’