Beki wa kati wa Yanga Dickson Job atakosekana katika mechi kipindi chote kilichosalia msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha taarifa hiyo ya kuwasononesha mashabiki wa Yanga ambao walitarajia kuona nahodha wao msaidizi anarejea mapema kikosini.
Kamwe amesema tathmini ya awali ilionyesha Job angekosekana kwa kipindi cha wiki 8 hadi 12 lakini baada ya kukamilisha mchakato wake wa matibabu huko Afrika Kusini, sasa atakosekana kwa kipindi chote kilichobaki msimu huu.
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kumuombea Job ili apone majeraha ili arejee akiwa imara zaidi msimu ujao.
Job anaungana na mshambuliaji Clement Mzize ambaye pia alifanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni huko Afrika Kusini.
Mzize nae atakosekana katika kipindi chote klichosalia msimu huu.