Zimbwe Jr aipania Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2026
Zimbwe Jr aipania Azam Fc

Mlinzi wa kushoto wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema licha ya ugumu wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, wamejiandaa kikamilifu ili kuondoka na alama tatu katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Zimbwe Jr ambaye amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipotua kwa mabingwa hao watetezi akitokea klabu ya Simba, amesema wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na dhamira ya kushinda na kuhakikisha hawaruhusu bao kama walivyofanya katika mechi zilizopita.

"Sisi kama wachezaji maandalizi yameenda vizuri, leo tutakuwa na nafasi ya kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho."

"Tunatambua ni mchezo muhimu, utakuwa mchezo mgumu kwa sababu tunakutana n wapinzani wagumu. Tuna imani na maandalizi yetu, nina uhakika wa asilimia 100, tunakwenda kufanya vizuri na kupata alama tatu."

"Nikiwa ni mchezaji ninayehusika kwenye eneo la ulinzi, jukumu letu la kwanza ni kuhakikisha haturuhusu goli, na tunatambua huu ni mchezo muhimu wa ligi hatutakiwi kupoteza hivyo tutapambana ili tuweze kutimiza malengo yetu," alisema Zimbwe Jr.

Yanga ndio vinara wa ligi kuu wakikusanya alama 35 kutoka mechi 13, Azam Fc inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 baada ya mechi 13

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’