Dube apata jeraha la nyama za paja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Mar 2026
Dube apata jeraha la nyama za paja

Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube jana alishindwa kumaliza mchezo wa ligi kuu dhidi ya TRA United baada ya kupata majeraha.

Daktari wa Yanga Dk Moses Etutu amethibitisha Dube alipata jeraha la nyama za paja 'hamstring' akitarajiwa kuukosa mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumamosi, March 21 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Kuumia kwa Dube kunaifanya Yanga iwakose washambuliaji wake wote wa kikosi cha kwanza wakiwa ni majeruhi.

Dube ameungana na Clement Mzize na Laurindo Aurelio 'Depu' ambao wote wanauguza majeraha.

Jeraha la Dube huenda likamuweka nje ya uwanja kwa muda wa hadi wiki tatu.

Jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji sasa limebaki kwa Emmanuel Mwanengo ambaye jana katika mchezo dhidi ya TRA United aliingia baada ya Dube kuumia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’