FT : Mtibwa Sugar 1-1 Yanga, NBC PL, March 21

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Mar 2026
FT : Mtibwa Sugar 1-1 Yanga, NBC PL, March 21

Bao la dakika za lala salama lililofungwa na Mtibwa Sugar kupitia mpira wa kona uliopigwa na Ismail Mhesa limewanyima Yanga alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Wachezaji wa Yanga walimlalamikia mwamuzi kwa kuruhusu bao hilo licha ya mlinda lango Djigui Diarra kuonekana amesukumwa wakati akijaribu kuokoa mpira huo wa kona.

Yanga ilikuwa na kwanza kufunga bao la uongozi kupitia kwa Pacome Zouzoua kwenye kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Emmanuel Mwanengo.

Hata hivyo wachezaji wa Yanga watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na alama tatu katika mchezo huo kwani walitengeneza nafasi nyingi lakini changamoto ilikuwa katika kuweka mpira kimiani.

Mwanengo angeibuka shujaa wa Yanga kwenye mchezo huo kama angefunga nafasi adimu aliyopata dakika za lala salama

Ni sare ya tatu mfululizo Yanga inapata, pengine ni nyakati ngumu zaidi kutokea kwa Yanga kwenye ligi katika misimu ya karibuni.

Msimu uliopita Yanga ilipoteza mechi mbili mfululizo lakini wakati huu sare tatu mfululizo, Yanga ikianza kwa kuchechea mechi za duru ya pili.

Yanga inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha alama 38, na kimahesabu wataendelea kuwa kileleni hata ikitokea timu nyingine zitashinda mechi zao za viporo.

Hiyo ilikuwa mechi ya 7 Yanga wanacheza katika kipindi cha siku 21

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
59m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’