Mkwasa ataja sababu ya 'kuficha' usajili wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jun 2018
Mkwasa ataja sababu ya 'kuficha' usajili wa Yanga
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema klabu hiyo itaweka wazi wachezaji inaowasajili baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili.

Mkwasa amesema vilabu vinavyofanya usajili sasa vinakiuka kanuni kwa kuwa dirisha la usajili bado halijafunguliwa.

"Unajua klabu zinazosajili hivi sasa zinaenda kinyume na utaratibu wa usajili, na hii yote ni kwasababu dirisha bado halijafunguliwa," amesema Mkwasa

Msimu huu Yanga imekuwa ikifanya usajili wake kwa usiri mkubwa tofauri na miaka mingine.

Ukiacha sababu iliyotolewa na Mkwasa, sababu nyingine ya kusajili kwa usiri ni kukwepa 'hujuma' zinazofanywa na baadhi ya timu.

Yanga haikufanikiwa kusajili wachezaji wote iliyokuwa imeweka wazi kutaka kuwasajili baada ya 'kuwahiwa' na timu nyingine.

Wachezaji kama Adam Salamba, Mohammed Rashid, Tiber John, Habibu Kiyombo na Marcel Kaheza kwa nyakati tofauti walihusishwa na Yanga lakini ni vilabu vya Simba na Singida United vilivyowasajili.

Mkwasa aliwahi kunukuliwa na gazeti moja la kila siku akisema kuwa wamebaini kuna timu zinasajili kwa kuitumia Yanga, zinasubiri Yanga isema inataka kumsajili nani.

Mkwasa amewahakikishia wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kongwe kuwa wako makini na zoezi la usajili.

"Mashabiki na Wanachama wetu wawe na subira. Wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’