Moalin kurudi na Gusa Achia Twende Kwao?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Mar 2026
Moalin kurudi na Gusa Achia Twende Kwao?

Klabu ya Yanga imetangaza kumrejesha Abduhamid Moalin kikosini kuwa kocha msaidizi akiungana na Kocha Mkuu Pedro Goncalves ambaye uongozi umeridhia aendelee na majukumu yake.

Baada ya tathmini ya kina kufanyika, uongozi wa Yanga umebaini timu imepoteza 'utambulisho' wake, ujio wa Moalin ni katika kujaribu kurejesha utambulisho huo.

Moalin alikuwa sehemu ya benchi la ufundi msimu uliopita ambao Yanga ilifanikiwa kuondoka na mataji matano.

Alianza majukumu yake kama Mkurugenzi wa ufundi na baadae kuwa Kocha Msaidizi akifanya kazi Sead Ramovic na Miloud Hamdi.

Sasa anakwenda kufanya kazi na Pedro ambaye sasa atalazimika kubadilika 'kimbinu' ili kwendana na utamaduni wa soka la Yanga.

Mpaka kufikia hatua hii ni wazi Pedro ameridhia kufanya kazi na Moalin ambaye kimsingi anajua vyema utambulisho wa soka la Yanga akiwa amefanya kazi na Ramovic wakiasisi 'Gusa Achia Twende Kwao' na Hamdi ambaye kimsingi aliendeleza pale alipoacha Ramovic.

Baada ya Ramovic kuondoka, Moalin aliongoza benchi la ufundi kwa muda kabla ya ujio wa Hamdi na wawili hao kuendeleza makali ya Yanga.

Chini ya Hamdi Yanga ilitoka sare mechi moja tu na kushinda zote zilizobaki wakitwaa ubingwa na rekodi ya alama nyingi (82) kuliko wakati mwingine wowote.

Moalin pia ana uzoefu mkubwa na soka la Tanzania, kabla ya kujiunga na Yanga alifanya kazi Azam Fc kama mchambuzi wa video, kocha msaidizi na baadae kuwa kocha mkuu.

Alipoondoka Azam Fc alijiunga na KMC kabla ya Yanga kumuajiri. Hivyo atakuwa msaada kubwa kwa benchi la ufundi hasa kwa mechi za ugenini.

Makocha wote ambao wako kwenye benchi la sasa la Yanga ni wageni, pengine wanashindwa kutumia mbinu sahihi katika mechi za ugenini na kupelekea Yanga kudondosha alama nyingi ugenini.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’