Mwanengo bado vitu vichache tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Mar 2026
Mwanengo bado vitu vichache tu

Kuumia kwa washambuliaji Clement Mzize, Laurindo Aurelio na Prince Dube kumetoa nafasi kwa mshambuliaji Emmenuel Mwanengo kutumika kwenye kikosi cha kwanza.

Katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa mkoani Dodoma na kumalizika kwa matokeo ya sare ya baao 1-1, Mwanengo alicheza kwa dakika zote 90.

Bao la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Pacome Zouzoua, pasi ilitoka kwa Mwanengo aliyewahi mpira uliotemwa na mlinda lango wa Mtibwa Sugar Constantine Malimi baada ya shuti la Allan Okello.

Mwanengo pia alifunga bao kwenye kipindi cha kwanza lakini lilikataliwa kimakosa baada ya mwamuzi msaidizi kutafsiri aliyetoa pasi bao hilo (Pacome) kuwa ameotea wakati haikuwa hivyo.

Lakini pia Mwanengo angeweza kuipa Yanga alama tatu dakika za lala salama kama shuti lake ndani ya 18 lisingeokolewa na mlinda lango wa Mtibwa Sugar.

Kukosa nafasi hiyo adimu dakika za lala salama pengine ndio iliyopelekea ashushiwe lawama za kila aina na baadhi ya mashabiki pasipo kuangalia mchango wake katika mchezo huo.

Kama angefunga nafasi ile pengine tuzo ya nyota wa mchezo angestahili kupewa yeye kutokana na kile alichofanya katika mchezo huo.

Eneo ambalo Mwanengo anapaswa kulifanyia kazi ni usahihi wa maamuzi na matumizi ya nafasi. Yaani aongeze ukatili mbele ya lango.

Ujio wa Mwanengo aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea TRA United, unaweza kuwakumbusha Wananchi wakati Clement Mzize alipopandishwa timu ya wakubwa na kocha Nasreddine Nabi.

Zipo nyakati Mzize alikumbana na ukosoaji sana kutokana na ufanisi wake mbele ya lango, lakini aliendelea kuaminiwa na kupewa nafasi mpaka kufikia hapo alipo.

Mwanengo pia ameanza vyema majukumu yake anachohitaji ni kuaminiwa na kupewa muda aweze kuimarika zaidi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’