Kikosi cha Yanga jana kilirejea rasmi mazoezini kujiandaa na mechi za kuhitimisha duru ya pili ligi kuu ya NBC pamoja na michuano ya kombe la CRDB.
Kabla ya kuanza mazoezi, waandishi wa habari wakapewa nafasi ya kufanya mahojiano na wachezaji, benchi la ufundi ikiwa pia siku maalum ya Media.
Baada ya zoezi hilo, jioni kikosi kikaanza rasmi program za mazoezi chini ya Kocha Mkuu Pedro Goncalves na Msaidizi wake Abdulhamid Moalin ambaye jana alianza rasmi majukumu yake.
Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumamosi, April 04 katika uwanja huo KMC Complex.
Baada ya kumaliza mechi za duru ya kwanza kwa kusuasua, Wananchi wamepania kurejea na kwa nguvu kuhitimisha mechi za duru ya pili kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.








